Kuhusu Sisi

Sisi ni Nani

Psiphon Inc. ni kampuni iliyoko Toronto, inayozalisha programu huria ya mifumo mingi inayosaidia zaidi ya watu milioni 3 kila wiki kuungana na maudhui kwenye Mtandao. Sisi ni timu inayolenga kutoa programu bora zaidi, kutambulisha bidhaa mpya mara kwa mara na kuhakikisha kuwa tunaendeleza mahitaji ya hadhira yetu inayokua kila mara ulimwenguni.

Timu ya Exec

Michael Hull ni Rais wa Psiphon Inc., na amekuwa na Psiphon tangu mwanzo, ilipoanza kama mradi katika Citizen Lab, Chuo Kikuu cha Toronto. Tangu wakati huo ameongoza juhudi za ukuzaji wa programu na husaidia kuendesha uvumbuzi ambao huiweka Psiphon kidedea kwenye fani yake.

Uundaji Mfumo

Katika Psiphon, tunahitaji watumiaji wetu kuwa na matumizi mazuri. Hii ina maana kwamba programu yetu inahitaji kuwa rahisi kutumia, mtandao wetu unahitaji kuwa wa haraka, na zote zinahitaji kuwa thabiti kama mwamba. Hili ni ngumu kwa wasanidi programu wowote kuafikia, lakini haswa wakati programu yako inapaswa kufanya kazi katika mazingira ya maadui yanayobadilika kila wakati na katika lugha na mifumo mingi.

Pia tunajua kuwa ni muhimu vile vile kufanya kazi kwa bidii kwa watumiaji wetu nyuma ya pazia. Tunalinda watumiaji wetu na data zao kwa kiwango kikubwa. Watumiaji huenda wasitambue hatua za kuhakikisha faragha na usalama wao, lakini tunajua wanaithamini.

Timu ya ukuzaji programu ya Psiphon inajitahidi kutoa masuluhisho bora zaidi, ya haraka zaidi, rahisi na yaliyo wazi zaidi. Pia tunachunguza maeneo mapya ambapo utaalamu wetu unaweza kulinda, kuwezesha na kukomboa mawazo ya watumiaji duniani kote.

Uendeshaji na Ufikiaji

Tuna kandarasi na kampuni mbalimbali, kutoka kwa watangazaji wakubwa wa kimataifa hadi mashirika madogo ya haki za binadamu yanayofanya kazi katika nchi fulani. Timu yetu ya Uendeshaji na Ufikiaji hukusanya ripoti zinazowaonyesha ni watu wangapi wanapata Psiphon kupitia mbinu zao za usambazaji. Pia wanasoma mienendo na kuangalia matukio yajayo ambayo yanaweza kuathiri mtiririko wa bure wa habari kwenye Mtandao.

Ushirika

Psiphon inafanya kazi kwa karibu na vikundi mbalimbali ili kutoa msaada na ushauri kwa watu wanaotumia Psiphon popote walipo. Tuna tafsiri za programu yetu katika lugha nyingi, na tunaongeza zaidi kwa bidhaa zetu kupitia Transifex, kwa usaidizi wa Localization Lab.

Wasiliana Nasi

Unaweza kuwasiliana na Psiphon kupitia kutuma barua pepe kwenda:

[email protected]

Pata habari za hivi punde kuhusu Psiphon  

Jiunge na orodha zetu za barua pepe: