Hukufikisha unapotaka kwenda...

Je, umedhibitiwa na nchi, shirika, au chuo chako?

Baada ya kushughulika na tawala kandamizi duniani kote, tunafaa kwa namna ya kipekee kukusaidia kufikia maudhui unayotaka, wakati wowote na popote unapoyataka.

Jinsi Psiphon Inafanya kazi »

...na kukufikisha salama.

Je, ungependa kuvinjari kwa usalama unapotumia WiFi ya umma?

Mtandao wa bure ni mzuri, lakini vidakuzi na akaunti zilizoibiwa sivyo. Psiphon hukupa njia salama ya Mtandao, haijalishi unatumia mtandao gani kuunganisha.

Nitawezaje kujua kama naweza kuiamini Psiphon? »

Uaminifu, Kasi, Urahisi: chagua tatu

Tangu 2008, Psiphon imesaidia mamilioni ya watu katika nchi zilizo na vikwazo vya uhuru kote ulimwenguni kufikia maarifa na mawazo yaliyodhibitiwa kwa usalama. Sasa Psiphon inaweza kukufanyia vivyo hivyo. 

Pakua Psiphon »

Psiphon ni nini?

Psiphon ni zana ya kukwepa kutoka Psiphon Inc. ambayo hutumia teknolojia ya VPN, SSH na HTTP ili kukupa ufikiaji usiodhibitiwa wa maudhui ya Mtandao. Kiteja chako cha Psiphon kitajifunza kiotomatiki kuhusu sehemu mpya za ufikiaji ili kuongeza uwezekano wako wa kukwepa udhibiti.

Kuhusu Sisi »